JINSI YA KUANZA KUTUMIA TUNZAA+

Tunzaa
4 min readSep 15, 2022

Kuuza bidhaa kwa njia ya mtandaoni ni changamoto hasahasa kama ni mara yako ya kwanza au kama huna ujuzi. Makala hii itakupa muongozo wa jinsi ya kuanza kutumia aplikesheni ya Tunzaa+ kuuza bidhaa zako.

Zama hizi za biashara zinapelekea kila mfanyabiashara kutafuta njia mpya za kuwafurahisha wateja wake na hivyo ni wakati sahihi kwako pia kuwafurahisha wateja wako kwa kufanya maamuzi muhimu kwa ajili ya biashara yako na kutumia majukwaa sahihi kuuza bidhaa na huduma zako.

Mitandao ya kijamii imeleta watu pamoja na watu wengi hivi sasa hufanya manunuzi mtandaoni, kama asemavyo Bill Gates “kama biashara yako haipo mtandaoni basi biashara yako ipo nje ya ulimwengu wa biashara”.

picha kutoka unsplash.com

Kujisajili katika aplikesheni ya Tunzaa+ ni bure! Unapata nafasi ya kuonesha bidhaa na huduma zako katika soko la Tunzaa+, kufatilia mauzo yako, na inakupa huduma bora kwa wateja na kuitangaza biashara yako bure kabisa.

Ni kitu gani utahitaji ili kujiunga na Tunzaa+?

Tunzaa+ inazingatia utoaji wa bidhaa na huduma zilizo katika ubora wa hali ya juu kwa wateja wake na kuhakikisha kila biashara iliyopo Tunzaa inakuwa imesajiliwa TRA. Hivyo basi unapotaka kujiunga Tunzaa+ hakikisha una leseni ya TRA, leseni ya BRELA na namba ya TIN ya biashara yako.

Unaweza kujiunga na familia ya Tunzaa+ hata kama bado hujasajili bishara yako, unachotakiwa kufanya ni kuruhusu Tunzaa+ iwakilishe bidhaa na huduma zako katika duka lake. Hii inawezekana katika njia mbili, ya kwanza, unaweza kuwauzia Tunzaa+ bidhaa zako kwa bei ya jumla au unaweza kuruhusu bidhaa zako ziwakilishwe na duka la Tunzaa+ huku wakikata asilimia chache katika mauzo ya bidhaa zako.

Tuanze sasa na Tunzaa+

  • Ni rahisi! Pakua na sakinisha Tunzaa+ kwenye simu yako ya kiganjani kupitia play store au Appstore
  • Sajili biashara yako. Usajili ni pamoja na kuweka taarifa muhimu na maelezo juu ya biashara yako.
  • Mara baada ya kumaliza usaliji wako, utapokea ujumbe mfupi kutoka timu ya Tunzaa utakao thibitisha usajili wako na kukuongoza katika kumalizia taratibu zilizobaki za usajili.
picha ya unsplash.com

Baada ya kuthibitishwa, utaanza matumizi ya aplikesheni kwa kuhariri ukurasa wako, kuweka maelezo muhimu juu ya bidhaa zako kuweka picha na bei za bidhaa na huduma zako. Huhitaji kuwaza sana, kama una maswali yoyote usisite kuuliza timu ya Tunzaa kwani ipo tayari kukusaidia na kukuongoza kuelekea njia ya mafanikio.

Tunzaa+ ina duka la kawaida ambalo linatumika kuunganisha wateja na wafanyabiashara. Wafanyabiashara wanapata nafasi ya kuweka bidhaa zao katika duka hili kwa ajili ya wateja kuweza kuziona na pia kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa kwa wateja walio karibu na duka hilo.

Tunzaa+ ina thamini maoni kutoka kwa wafanyabiashara wanaotumia aplikesheni hii, kwani ni njia sahihi ya kupata na kuelewa mahitaji tofauti ya kila mfanyabiashara na kuyafanyia kazi.

Kutana na Outreach bin masters, wamekuwa wakitumia Tunzaa+ kwa mda wa mwaka mmoja sasa na wamekuwa wakifurahishwa na ongezeko la wateja tokea waanze kutumia aplikesheni ya Tunzaa+. Outreach wanasema,

“Kwa mara ya kwanza tuliisikia aplikesheni ya Tunzaa+ kupitia twitter na tumekuwa tukifurahia huduma zinazotolewa na timu ya Tunzaa+”

Timu ya Tunzaa+ ipo tayari kutoa msaada kwa wakati wowote unapohitajika ili kuhakikisha wafanyabiashara na wateja wake wanapata huduma zenye ubora wa hali ya juu.

Unachokihitaji kwa sasa katika biashara yako ni kuwa na aplikesheni ya Tunzaa+, njia sahihi ya kukutana na wateja wako na kuwafanya wajihisi wa kipekee huku ukitengeneza faida kubwa. Kuwa mwanafamilia wa Tunzaa+ kwa kufata hatua hizi chache na wakati wowote unapo hitaji msaada, usisite kuwasiliana nasi.

Imeandikwa na Anthonia Koba

Imehaririwa na kuhakikiwa na Asmin Gombo, Queenlisajoan Olan’g na David Shughuru.

--

--

Tunzaa

Tunzaa is a fintech product that improves financial habits of everyday Africans through gamification with a marketplace for goods & services.