NJIA YA KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA YAKO

Tunzaa
5 min readAug 1, 2022

Kuwepo kwa idadi kubwa ya majukwaa ya kufanyia biashara mtandaoni kumerahisisha sana uuzaji wa bidhaa na hivyo kupelekea ongezeko la ushindani hasahasa kwa biashara zinazouza bidhaa zenye mfanano. Utawezaje kuuza bidhaa zako kwa wateja wengi zaidi na kupata wateja wa kudumu?

Jibu la swali hili ni TUNZAA+. Aplikesheni inayokupa jukwaa la bure utakalolitumia kuorodhesha bidhaa, kuuza na kupokea malipo papo kwa papo au kwa awamu.

Lengo kuu la Tunzaa+ ni kutoa fursa kwa wafanyabiashara kuweza kufikia kundi kubwa zaidi la wateja na pia kutengeneza soko la kidigitali linalowapa nafasi wateja kufanya malipo kidogo kidogo na hivyo kubadilisha tabia zao kifedha. Kujisajili Tunzaa+ na kuorodhesha bidhaa zako ni bure kabisa, utalipa kiasi kidogo cha ada pale tu utakapo uza kupitia Tunzaa+, Ada hii itatumika kulipia shughuli za malipo na operesheni za kibiashara.

Tunzaa+ inalenga katika utoaji wa huduma bora na zenye kuaminika, ndiyo maana kila biashara inayosajiliwa Tunzaa+ inatakiwa kuwa na leseni ya TRA ili kuambatana na sheria na kanuni za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunzaa+ inashirikiana na kampuni kama TIGO, SAMSUNG, HISENSE, WESTPOINT, MKUKI NA NYOTA, AFRIMED, MARS COMMUNICATIONS, PINPOINT ELECTRONICS, ZARA ADVENTURES TANZANIA, BAOBAB SAFARI CONSULTING COMPANY, MASHIRIMA TOURS, na nyingine nyingi ili kuhakikisha inatoa huduma bora na bidhaa zenye viwango vya hali ya juu.

Kwa sasa Tunzaa ina zaidi ya watumiaji 13k na imepokea oda zaidi ya 1800, Takwimu zinaonesha tokea kuanzishwa kwa Tunzaa+ wachuuzi waliosajili biashara zao, wamepokea wastani wa M6.5

Tunzaa inafanyaje kazi?

Tofauti na majukwaa mengine, Tunzaa huwapa wateja wake kipaumbele cha kufanya maamuzi kati ya kulipia papo kwa papo au kufanya malipo kidogo kidogo, kupitia njia hii, mfanya biashara anapata nafasi ya kuuza bidhaa zake kwa kundi la wateja ambalo ni jipya na kubwa zaidi na hivyo kuwapa wateja kile wanachohitaji.

Kujisajili Tunzaa+ ni rahisi!

Pakua na sakinisha aplikesheni ya Tunzaa+ iliopo katika mfumo wa Android na iOS

Sajili biashara yako na kuweka taarifa muhimu kuihusu biashara yako

Utapokea ujumbe wa uthibitisho mara baada ya timu ya Tunzaa+ kuhakiki usajili wako.

Anza safari yako kwa kuweka bidhaa zako, bei na kuhariri ukurasa wako.

Ili kuweza kufatilia na kuhifadhi shughuli za wateja wako kwa urahisi, Tunzaa+ itahakikisha unapokea ujumbe mfupi utakao kutaarifu juu ya kila oda au malipo yatakayofanywa na wateja wako.

Mafanikio yako yatachangiwa na juhudi zako katika kutengeneza ukurasa bora katika jukwaa la Tunzaa+. Je unatengenezaje kurasa yenye mvuto kwa wateja?

Pakia picha zenye ubora wa hali ya juu ili kumsaidia mteja kutambua bidhaa yako kwa urahisi na kuepusha mkanganyiko.

Tengeneza urahisi kwa mteja kupata kile anachokitafuta kwa kuandika kichwa cha habari kinacho husiana na bidhaa unayouza, pia, unapoandika kichwa cha habari kinachohusiana na bidhaa yako unaitengenezea nafasi nzuri biashara yako kuonekana kwa urahisi.

Katika kila bidhaa utakayo orodhesha, hakikisha unaambatanisha maelezo sahihi kuhusu bidhaa yako ili kumpa mteja wepesi katika kuielewa bidhaa hiyo. Mwisho, weka bei sahihi zitakazo endana na soko la bidhaa unayouza. Hivyo basi, utakapo fatilia pointi hizi chache katika utengenezaji wa ukurasa wako Tunzaa+, utakuwa katika nafasi nzuri kupata wateja wa uhakika na wa kudumu.

Jitofautishe na wengine kwa kufanya maamuzi ya kupakua aplikesheni ya Tunzaa+ sasa! Ipe biashara yako thamani inayo stahili.

Kwanini Tunzaa?

Ni njia sahihi ya kukuza biashara yako, kwa sababu inakupa nafasi ya kuhudumia wateja wapya, tofauti na wenye hamu ya kufanya manunuzi.

Utumiapo Tunzaa+ sio lazima kuwa na duka la kawaida bali unaweza kuuza mtandaoni na kuwasilisha bidhaa zako katika duka la Tunzaa ili ziwafikie wateja wako kwa urahisi.

Tunzaa+ inahakikisha uwasilishaji salama wa malipo kutoka kwa mateja kwenda moja kwa moja kwa mfanyabiashara. Watumiaji wengi wa Tunzaa+ hujivunia kutumia aplikesheni hii kwani inaziongezea thamani biashara zao na kuzifanya zikue kwa kasi.

image from unsplash.com

Pia aplikesheni hii ni rahisi na salama kwa matumizi na humpa mfanyabiashara uhuru wa kufatilia wateja wake na kuongeza bidhaa mpya kwa wakati wowote.

Kama asemavyo mwandishi maarufu Ken Blanchard

“maoni/marejesho ndo kifungua kinywa cha mabingwa/bingwa”

Tunzaa+ imekuwa mstari wa mbele katika kupokea na kutoa maoni kwa watumiaji wake.

Kutana na iFRESH General Solutions mmoja kati ya wateja wetu wa kwanza kabisa kujiunga na Tunzaa+. Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya mahojiano na ifresh gerenal ili kujua jinsi gani Tunzaa+ imekuwa na msaada katika biashara yake.

“Tunzaa+ imesaidia kuniunganisha na wateja wanaofanya malipo kidogo kidogo. Nimeifahamu Tunzaa kupitia mtandao wa Twitter na tokea hapo nimekuwa nikiwaelimisha wateja wangu juu ya Tunzaa, hasahasa wale wanaoomba punguzo la bei”

Ifresh General imeridhishwa na huduma zitolewazo na Tunzaa+ na kuongezea kuwa

“aplikesheni hii imerahisihsa mambo mengi kwenye biashara yangu na ni rahisi kutumia”.

Ifresh General Solutions ni wauzaji wa vifaa asilia vya kutunza ndevu. bidhaa zao zinafaa kwa matumizi na hazibagui nywele za aina yoyote. kuanzia mafuta ya kukuza ndevu mpaka sabuni ya kuoshea nywele na ndevu, bidhaa zao zina ubora wa hali ya juu.

“ Sijapata na vikwazo vyovyote tokea nijiunge Tunzaa+ mwaka 2021 na sababu kuu iliyonifanya nijiunge na aplikesheni hii, kwanza imeanzishwa na kijana mwenzangu wa kitanzania lakini pia ni jambo zuri katika biashara hasahasa biashara yangu”

Huu ni wito kwa wafanyabiashara wote Tanzania/Africa, wakati sahihi umefika wa kupanua biashara yako kwa njia ya kipekee. Jiunge sasa na Tunzaa+ ili uweze kufikia mtandao wa wanunuzi ambao wako tayari kufanya manunuzi kutoka kwako. Usisite kuwasiliana nasi https://linktr.ee/Tunzaa

--

--

Tunzaa

Tunzaa is a fintech product that improves financial habits of everyday Africans through gamification with a marketplace for goods & services.